HALLELUJAH

BWANA YESU KRISTO ASIFIWE! Nakusalimu mtu wa Mungu. karibu katika ukurasa huu maalumu kwa ajili ya mafundisho ya Neno la Mungu, naamini utajifunza na kujengeka kiroho.

"Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkishukuru Mungu Baba kwa yeye."
wakolosai 3;16,17

Wednesday, 24 August 2016

MAMBO YA KUTAFAKARI KABLA YA KUFANYA UAMUZI WA KUOA AU KUOLEWA

MAFUNDISHO MAALUM KWA VIJANA

By 
Mwalimu Christopher Mwakasege
Wiki ya Saba
Jambo la Saba; Je! Uko tayari kuoa au kuolewa?
Ni swali muhimu, uko tayari, maana yake umefika mahali hali yako ya ndani na nje, inakuruhusu kuoa au
kuolewa? Uko tayari kuoa au kuolewa? Umefika mahali pa namna hiyo?. Wengine wanasema huyu ni mtoto, lakini unajua pamoja na kwamba ni mtoto, ni vizuri kujua kama uko tayari kiumri. Lakini ninapozungumzia hapa juu ya utayari wa kuoa au kuolewa, sizungumziitu habari za miaka, bali ninazungumzia habari za hali yako ya ndani.Nimeona kuna mtu mwingine ana miaka arobaini, lakini kwa kweli hayuko tayari kukaa na mwanamke, ndani yake, mawazo yake na kufikiri kwake, hayuko tayari kukaa na mwanamke, hawajibiki hata yeye mwenyewe juu yake mwenyewe. Wengine hata wana miaka hamsini, lakini ana hali kama hii. Nimeona akinadada hata wana miaka arobaini na tano, hayuko tayari kuolewa, maana akiolewa ni shida tu.
Nilienda mahali fulani, nikakuta dada ana umri mkubwa tu, lakini wakati wa maombi hakusema kama anataka tuombe ili aolewe. Nikaona ngoja nimuulize labda anaona aibu kusema hitaji hili kwa sababu umri umesogea, nikamwambia “hutaki tuombe uolewe”? Akasema, “hapana, sitaki kuolewa” (Na alikuwa ana umri wa miaka kama arobaini na zaidi). Nikamuuliza, “kwa nini”.
Akasema, “kwa sababu sitaki kuomba ruhusa kwa mwanaume ninapotaka kutumika”. Nikamuuliza unafanya kazi, akasema, “ndio”.
Nikamwambia, “unapokwenda kumtumikia Mungu huwa unafanyaje, - unaomba ruhusa au unatoroka huko kazini?” Akasema, “ninaomba ruhusa”. Nikwamwambia, “kwa nini unaona ni rahisi kuomba ruhusa kwa mwajiri wako na unaona taabu kuomba ruhusa kwa mume wako?” Alishindwa kujibu hilo swali. Nikamwambia tatizo lako ni kubwa kuliko unavyo fikiri.
Unaweza ukaona kabisa ya kwamba, huyu mtu hayuko tayari kuolewa, wala msijaribu kumlazimisha aoelewe – pamoja na kwamba umri wake ni mkubwa. Usijaribu kumsukuma kwenye maamuzi ya kuolewa maana hayuko tayari kuolewa, akiingia kwenye ndoa atakwenda kuleta shida
tu! Ndio maana ninakuuliza swali, je uko tayari kuoa au kuolewa? Lina vipengele vingi vya kulitazama, na linabadilisha vitu vingi sana.
Mwingine unakuta ni msichana, wazazi wake ndio wanamtegemea karibu katika kila kitu.
Mimi ninakuambia kabla hujafikiria kuoa au kuolewa, fikiria hilo swali. Kwa sababu ukiishaolewa tu biblia inakuambia wasahau watu wa nyumbani mwa wazazi wako (Zaburi 45:10). Sasa haimaanishi usiwasaidie, ila maana yake ni kwamba huwezi ukawasaidia tena ‘moja kwa moja’
kama ulivyokuwa unawasaidia zamani. Ni vitu lazima ujadiliane na mume wako juu ya kuwasaidia wazazi wenu wa pande zote mbili – maana mna mipango yenu sasa.
Na inawezekana labda umeoa au umeolewa kwa kijana ambaye hana mzigo na wazazi wake kabisa, kila mtu anaishi kivyake vyake kama simba  porini, suala la kusaidia wazazi hana ndani ya moyo wake. Wewe umekuwa na huo mzigo, wazazi wako wamekulea, umefika mahali umeanza kazi, sasa na wewe unawatunza hatua kwa hatua, siku unaolewa yule baba anasema basi
usiwatunze tena, - fikiri hilo.
Litakuwa linakuumiza kila siku jinsi wazazi wako wanavyopata shida. Utafika mahali utakuwa unachukua vitu kisiri siri unapeleka kwa wazazi, na hiyo ina shida yake pia. Kwa hiyo kabla hujakubali kusema mimi nataka kuolewa, fikiri kwanza na kuomba, maana ndoa inakwenda kukubadilishia mambo yako mengi.

No comments:

Popular Posts

Pageviews

WASILIANA NASI

Name

Email *

Message *