MAFUNDISHO
MAALUMU KWA VIJANA
By
Christopher
Mwakasege.
Wiki
ya Nne
Jambo
la Nne
Uamuzi wa kuoa au kuolewa ni muhimu uwe mwangalifu nao,kwa sababu
utakufanya uwajibike zaidi.
Kama hujawa mtu wa kuwajibika, basi, hujawa tayari kuwajibika, kwa hiyo usiingie kwenye ndoa! Kuoa au kuolewa kunakufanya uwajibike zaidi, maana yake ni kutafuta wajibu mkubwa zaidi.
Kama hujawa mtu wa kuwajibika, basi, hujawa tayari kuwajibika, kwa hiyo usiingie kwenye ndoa! Kuoa au kuolewa kunakufanya uwajibike zaidi, maana yake ni kutafuta wajibu mkubwa zaidi.
1Timotheo 5:8 anasema,“Lakini mtu ye yote
asiyewatunza walio wake, yaani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana
Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiye amini”, maana yake ni mbaya kuliko
mtu ambaye hajaokoka. Afadhali mtu yule ambaye hajaokoka.
Huyo ambaye ameokoka, lakini hatunzi watu wa
nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, maana yake amemkana Yesu; ni mbaya
kuliko hata mtu ambaye hajaokoka.
Hii inaonyesha ya kuwa unaweza ukaingia kwenye ndoa
ukapoteza wokovu wako, ukakosa kwenda mbinguni, si kwa sababu umefanya
dhambi ya uasherati, lakini kwa sababu umeshindwa kutunza watu wa nyumbani
mwako, na kwa ajili hiyo unahesabika kuwa umeikana imani. Ukiangali kwenye
Tito.2:3-5 anasema,“Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa
utakatifu, wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao
mema, ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda
watoto wao, na kuwa wenye kiasi, na kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao,
kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe, ili neno la Mungu lisitukanwe”.
Unaweza ukaona kabisa ya kwamba Timotheo,
anazungumza habari za vijana wa kiume waliooa na wanafamilia, au umeoa na
hujapata mtoto. Unao watu nyumbani mwako, inawezekana
ni msichana umeolewa, huumstari pia unakubana.
Ukienda kwenye kitabu cha Tito, Tito anaandika moja kwa moja habari za
wanawake wazee, ili wawasaidie wanawake vijana, maana yake wasichana
ambao ndio wameolewa tu. Anasema,“Wawatie wanawake vijana akili, wawapende
waume zao na kuwapenda watoto wao”. Usingetegemea msichana aambiwe
awapende watoto wao, hutaona mwanaume anaambiwa awapende watoto, bali
anaambiwa awalee watoto. Mwanamke anaambiwa awapende watoto, ni kitu
ninashangaa kila siku; maana nisingetegemea mama aliyepata uchungu wa kuzaa
aambiwe ampende mtoto. Watu waliookoka wengi hasa wanapoingia kwenye ndoa,
wanaingia kienyeji -kienyeji tu, hawajali ya kwamba kuna kuwajibika.
Huwa ninawaambia vijana siku zote, hata kama
mlikuwa mmezoea kutokula nyumbani mwako, (maana kijana akiwa bado hajaoa,
anaweza akakaa wiki au wiki mbili, jiko lake halijawahi kupika kitu); kijana
akiwa bado hajaoa, hakimsumbui ana hela au hana hela, ataishi.
Chakula kikiisha anaenda kutembelea ndugu na jamaa, kama hawataki kumpa
chakula, atakaa hapo mpaka amekula na ndipo aondoke. Akikosa kabisa
atajitia moyo kwa Bwana kwamba amefunga, na kumbe ameshinda njaa!
Wakati mwingine mambo yakimzidia, na hana sabuni ya
kufulia nguo anasema hajali, kwa hiyo anaendelea, hana shida, anabadilisha
nguo sio kwa sababu amefua, lakini anabadilisha ili angalao jasho liweze
kupungua hasa mnuko wake, kwa hiyo anaitundika mahali ipigwe upepo usiku;
na baada ya siku mbili anavaa hiyo hiyo tena!
Huwa ninawaambia vijana siku zote kama hauko tayari
kuwajibika, usioe. Kwa sababu kama umeoa, haijalishi ya kwamba unafunga au
hufungi, chakula lazima kiwemo nyumbani mwenu. h haleluya! Na ukishaoa tu,
maana yake umeitangazia dunia nzima ya kuwa umeamua kuwajibika, na unaweza
ukatunza mke. Mambo ya kwenda kuomba -omba msaada tena inakuwa ni kitu
ambacho si wakati wake sasa. Maana unaposema, mimi nimeamua kuoa, maana
yake umekubali kuwajibika –na hii ni pamoja na kumlisha na kumtunza mke
wako.
Ndio maana ukienda kwenye makabila mengine
wanakuambia, ‘kijana unataka kuoa umejenga nyumba?’ Nimeona makabila
mengine wanauliza, ‘kijana wewe utaoaje wakati hata nyumba huna?’ Ndio maana
vijana wanazuiwa kuoa wakiwa shule, kwa nini, kwa sababu katika ndoa
watahitaji kuwajibika. Sio kwa sababu wakiwa shule hawawezi kuoa, ila ni kwa
sababu wanajua suala la kuoa sio kitu cha mchezo, linahitaji mahali ambapo
unahitaji kuwajibika. Ndani yako lazima uwe umekubali kuubeba wajibu
uliomo katika ndoa!
Na kama ni msichana unataka kuolewa ukubali
kuwajibika basi la sivyo usikubali kuolewa kama hujawa tayari kuwajibika.
Tito anawaambia wazi kabisa, ya kuwa wafanye kazi nyumbani mwao wenyewe.
Lakini sasa unataka hata kama umeolewa, uishi maisha kama msichana, na
hiyo ni hatari sana. Ukiingia kule ndani ya ndoa kuna mabadiliko. Wakati
ule ulikuwa unaosha vyombo vichache maana ni vya kwako peke yako, sasa na
mume wako yuko, na marafiki zake wamekuja –vyombo vya kuosha vitaongezeka, na
kuwajibika kwakokunaongezeka.Ilikuwa inakusumbua kupika, unapika mara moja
kutwa, na siku hizi wataalamu wametuletea kitu kinaitwa ‘hot pot’, kwa
hiyo hii mambo ya kupasha pasha moto chakula siku hizi wakati mwingine
hayahitajiki. Mtu ameweka chakula chake anakifunika vizuri, anakuja
jioni anakuta bado cha moto. Lakini ninakuambia labda umeingia umeolewa na
mtu ambaye ni mtumishi, ana wageni nyumbani kwake kama kituo cha polisi,
kila baada ya dakika mbili amekuja na wageni wengine.
Labda mume wako ni mkarimu sana, kila mgeni akija
anakuambia, “fulani chai vipi?” Huko jikoni ‘unauma vidole’ maana
umeshaingia jikoni kuanzia asubuhi; labda saa hiyo ni saa tano, na
umeshaingia jikoni kupika mara nyingi, maana wageni wanapishana kila
wakati. Kila saa ‘chai, chai’, unatamani uondoke ili usiendelee kupika,
lakini umebanwa – ndio kuolewa kwenyewe huko. Ukiamua kuolewa kuwajibika
kwako jikoni kutoangezeka zaidi.Huwezi ukaamua tu saa yoyote ukasema, mimi
nataka kwenda kutengeneza nywele, huo muda wa uhuru wa jinsi hiyo
umekwisha, ukitaka kwenda kutengeneza nywele lazima uage, huwezi
ukaondoka tu saa yoyote unayotaka, kila kitu
kinabadilika. Kuna masuala ambayo utahitaji kuwajibika nayo pale nyumbani,
huwezi kukwepa! Na kuna mambo mengine hakuna mtu mwingine ambaye atafanya
kwa niaba yako; kama usipotaka kuyafanya wewe. Ndio maana watu wanafika
mahali, msichana anaolewa lakini wiki ya kwanza tu anataka msichana wa
kazi wakati, hana hata mtoto mdogo. Unataka msichana wa kazi wa nini, huo ni
uvuvi
tu. Lazima uwe mwangalifu, wewe umeolewa tu,
unataka msichana wa kazi, wa nini? Unaweza ukajitetea na kusema ni
kukusaidia kazi - kazi zipi? Unaweza ukajitetea na kusema, aa!
Unajua ninachelewa sana kutoka kazini, angalao nikute mtu wa kupika. Mimi
ninakumbia unaanza vibaya. Kama ndiyo kwanza umeolewa tu, na unataka
wakumpikia chakula mume wako awe ni msichana wa kazi, basi unaanza vibaya.
Wakati huo ndio saa ya kumtayarishia mume wako
mapishi ambayo hajawahi kuona kwenye nyumba ya baba na mama yake! Akikaa
mwenyewe huku anakula awe anasema, ‘ahsante Yesu kwa kunipa msichana wa
namna hii!’ Kwa sababu hajawahi kuona chakula kizuri cha namna hiyoulichompikia
- hata hoteli hajawahi kukipata!
Lakini unaanza tu maisha ya ndoa na kumbandikia
mume wako watu wa kumhudumia, mimi ninakuambia unaanza vibaya, huko
unakoelekea na ndoa yako sio kuzuri. Uamuzi wa kuoa au kuolewa
usiucheezee, kaa chini, fikiri kwanza na kuomba kabla hujaamua.
Tunaomba radhi hatujafanikiwa kupata sehemu ya kwanza, ya tatu na ya tano.....tutaendelea na jambo la sita hadi la kumi na moja
No comments:
Post a Comment